1.0 UTANGULIZI
Jumapili ya Leo neno la Mungu linatukumbusha kuwa Roho mtakatifu ni Msaada wetu katika maisha yetu.
Roho Mtakatifu anatuwezesha kila Mkristo, bila kuzingatia, umri,jinsia au hali ya mtu katika jamii, ili kutoa unabii, kuota ndoto, na kuona maono.
Roho Mtakatifu anawashukia waumini wote ili kutusaidia kufanya kazi ya Mungu hapa duniani na kutulinda ( Kut 31:2 -3, Hes 11:29, Zab 51:11)
Roho mtakatifu ni muhimu sana katika kanisa la Mungu kwa sababu anatusaidia kuishi maisha matakatifu na kutimiza mpango wa Mungu katika maisha yetu..
Katika unabii ambao tumeusoma kutoka kitabu cha Yoel tunaona kuwa ulitimia siku ilie ya Pentekoste na Petro aliyarudia maneno haya (Mdo 2:16 – 21)
Katika unabii huu tunajifunza mambo kadhaa
2.0 ROHO MTAKATIFU YUPO KUWASAIDIA WATU WOTE
Yoel anatabiri kuwa Roho atawashukia watu wote na rika zote ili kuwasaidia, ili Mkristo uweze kusaidiwa unapaswa kutulia katika utakatifu na Roho Mtakatifu aweze kukupa Muongozo sahihi.
Ukiwa umefanikiwa sana usiache kumtumikia Mungu kwa sababu bado kuna mazuri zaidi ya hayo yapo mbele yako ambayo Mungu amekuandalia.
Ukiwa katika mateso, maumivu na changamoto za dunia usikate tamaa sababu bado kidogo kuna siku njema zinakuja ambazo Mungu amekuandalia.
3.0 HATARI IPO KWA WALE WATAKAOMKANA ROHO MTAKATIFU
Yoeli anatukumbusha kuwa ipo siku ya Hukumu inayokuja mbele yetu na kwa wale maadui wote wa Mungu siku hiyo itakuwa mbaya sana kwao sababu yatatokea mambo mengi ya ajabu.
4.0 KILA ATAKAYEMKUBALI ROHO MTAKATIFU ATAOKOLEWA.
Neno la Mungu linatuhakikishika kuwa pamoja na dhambi nyingi kuongezeka na watu kumuacha Mungu ila wapo watu ambao bado wataendelea kumtegemea Mungu na anasema hao wote ambao wataendelea kumtegemea wakimuita jina lake hakika atawaokoa.
5.0 HITIMISHO
Kila Mmoja atulie katika maongozi ya Roho Mtakatifu ili tupate kulindwa na kuelekezwa katika maisha ya Utakatifu.
AMEN.