All posts by Evangelist John(Charles)

Usharika wa uwemba wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania dayosis ya kusini karibu mbarikiwe pamoja nasi

KIPIMO CHA IMANI

Tangu nimeokoka nimebahatika kusikia mafundisho mengi sana mazuri kuhusu imani, wakati mwingine nilijifunza kuwa huhitaji imani kubwa kung’oa mlima, na nilipoijaribu imani ndogo kung’oa mlima, mlima uliishinda imani yangu ndogo. Je! Wapi hasa nilikosea mpaka kushindwa kuung’oa mlima mkubwa kwa imani ndogo? ( nadhani nilihitaji imani inayokua kama mbegu ya haladali, mpaka kuzidi ukubwa wa mlima ndipo niung’oe)

Leo ninataka kukueleza kipimo cha imani yako kwa maelezo haya.

Kama imani yako ya kufa ni kubwa kuliko ya kuishi basi jua huna imani au imani yako ni haba, hivyo kikubwa lazima kishinde kidogo.

Kama imani yako ya kutokupona ina nguvu kuliko kupona basi huna imani, au imani yako haba na chenye nguvu kitashinda.

Kama imani yako ya kukosa ni hakika kuliko ya kupata basi imani yako ni ndogo hivyo kukosa kutashinda, na kama imani yako ya laana ni zaidi ya baraka nakuhakikishia kila utakapoongea, utakachowaza, utakachoota, utakacokiona na kukikiri kitakuwa ni laana, balaa, mikosi na chenye nguvu kwenye akili yako, moyo wako na kinywa chako ndicho kitakachoshinda na kutokea kwenye maisha yako.

Nadhani umeshajipima kwenye eneo lako, sasa ni kazi yako kuhakikisha unaifanya imani yako iwe kubwa kuliko, mlima, magonjwa, madeni, na mahusiano ndipo utakapoweza kubadilisha mwonekano wa kinachokutisha kwa imani. KUMBUKA CHENYE NGUVU, UZITO, NA UHAKIKA NDICHO HUSHINDA.
Wakati wewe unaona haiwezekani kuna watu imewezekana, tofauti yako na yao ni kile unachokiona kigumu wao walikiona chepesi. Iga mwenendo wao utafanikiwa
@official_evjohn
#victoriousyear2020

WAJIBU WAKO

UNAWAJIBIKA NA MAISHA YAKO MWENYEWE. “Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe.” (Wagalatia 6:5) “Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari/hesabu zake mwenyewe mbele za Mungu.” (Warumi 14:12) “Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake.”
(Ezekieli 18:20)

Kwa msisitizo wa kipekee kabisa maandiko haya yanatuonesha kwamba kila mtu anawajibika na maisha yake mwenyewe. Hata mbele za Mungu hakuna atakaye hukumiwa kwa dhambi za mtu mwingine. Kwa maana hiyo hiyo basi hakuna anayewajibika na maisha ya mtu mwingine. Kwa mujibu wa maandiko haya ni makosa makubwa kuwa na MAWAZO TEGEMEZI, AKILI TEGEMEZI. Ile dhana ya KULAUMU WATU KWA SABABU HAWAJAKUSAIDIA inakemewa vikali na maandiko haya.
Simama upiganie maisha yako mwenyewe sio lazima watu wakusaidie hata kama uwezo wanao. Jukumu la kwanza la Baba yako ni kwa mke wake. Wewe ukishafika Miaka 18 unapaswa kuwaza kesho yako itakuwaje. Jukumu kubwa la Kaka na Dada zako ni maisha yao na watoto wao. Wewe sio jukumu lao. Acha kulaumu watu na usimame kutengeneza maisha yako mwenyewe.

Kama unataka kufunga Ndoa fanya unachomudu, usijiwekee bajeti kubwa kwa kuangalia mifuko ya watu. Kama hauna fedha achana na kusherekea Birthday, kunywa maji mshukuru Mungu. Kama umekosa kodi kalale kanisani saidiana na mlinzi ukiumwa mbu utapata akili ya kutafuta hela. Lakini usiwe mzigo kwa mtu yeyote na kulaumu na kuchukia watu. “Oh hawanisadii chochote!” Nani alikwambia unapaswa kusaidiwa!? KASIRIKA, CHUKIA, NUNA LAKINI UJUMBE NDIO UMEUPATA, PIGANIA MAISHA YAKO. KAMA AMBAVYO UTAHUKUMIWA KWA DHAMBI ZAKO MWENYEWE BASI VIVYO HIVYO AMUA KUFANIKIWA KWA JASHO LAKO MWENYEWE. -evjohn whatsup 0767386606
#2020

SIJAVIZOEA

SIJAVIZOEA.: 1 Samweli 17:38 Ndipo Sauli akamvika Daudi mavazi yake ya vita, akamtia chapeo cha shaba kichwani, akamvika dirii. 1 Samweli 17:39 Naye Daudi akajifunga upanga juu ya mavazi yake, akajaribu kwenda; maana alikuwa hajavijaribu. Daudi akamwambia Sauli, SIWEZI KWENDA na VITU HIVI, MAANA SIKUVIJARIBU (SIJAWAHI KUVITUMIA/SIJAVIZOEA). BASI DAUDI AKAVIVUA. 1 Samweli 17:40 AKAICHUKUA FIMBO YAKE MIKONONI, AKAJICHAGULIA MAWE LAINI MATANO KATIKA KIJITO CHA MAJI, AKAYATIA KATIKA MFUKO WA KICHUNGAJI ALIOKUWA NAO, MAANA NI MKOBA WAKE, NA KOMBEO LAKE ALIKUWA NALO MKONONI MWAKE, AKAMKARIBIA YULE MFILISTI. Mara nyingi huwa tunasubiri Mungu atupe wazo jipya la biashara au namna mpya ya utendaji ili tuweze kufanikiwa na tunasumbuka sana kuiga mifumo ya watu wengine na kuacha kuboresha kile ambacho tunakijua na kufanya kwa ubora tunasubiri wazo jipya na namna mpya ili kufanikiwa na kujikuta tunajichelewesha. Nimegundua mara nyingi sana Mungu huwa anatumia kile tunachokijua na kukiboresha ndipo hapo anatufanya kuwa bora na tofauti. Anamuuliza Musa “BWANA akamwambia, Ni nini hiyo uliyo nayo mkononi mwako? Akasema, NI FIMBO. Akamwambia, Itupe chini; akaitupa chini, nayo ikawa nyoka; Musa akakimbia mbele yake.” (Kutoka 4:2-3) Kipawa hicho unachokidharau, huduma hiyo hiyo unayoichukulia kawaida, biashara hiyo hiyo ya kawaida, ujuzi na uwezo ulionao ndio Mungu huwa anatumia kukufanya kuwa Mkuu. Usitafute sana kubuni ndege nyingine wakati unaweza kuboresha hii iliyopo na ukatajirika. USIHANGAIKE KUFUNGUA CHAMPAGNE 🍾 NA VIDOLE WAKATI UMEZOEA KUFUNGUA SODA KWA MENO, TUMIA UJUZI WAKO, ANAYEKUONA MSHAMBA NI KWA SABABU ANA NAMNA YAKE YA KUFANYA. KUWA BORA KATIKA NAMNA YAKO. – Ev.john

TAFAKURI YA JUMATANO YA MAJIVU 26/04/2020

Kesho nisiku pekee ambayo kanisa linaingia majira mapya yanayoitwa Kwaresma nasisi kama KKKT doyosisi ya kusini tunatoa tafakari fupi ya JUMATANO YA MAJIVU Jumatano ya majivu ni siku ya kwanza kwenye kipindi kiitwacho kwaresma ambapo siku hii inatukumbusha wakristo ya kwamba sisi ni mavumbi na mavumbini tutarudi kadiri ya agizo la Mungu katika mwanzo3:19 …….” hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi” Shabaha ya kuwekwa kwasiku hii nikutaka kuamsha akili za waumini ama washarika kutambua nafasi ya toba katika maisha haya mafupi Jumatano ya majivu kwamakanisa mengine kama oxthodox na katoliki huwapaka waumini wao majivu katika paji la uso wao ili kuwakumbusha inatupasa tuwe watu watoba lakini hiyo niishara ya nje ambayo hata mitume na manabiib waliitumia wakati wakifunga walivaa magunia nakujipaka majivu kuonyesha wanaomboleza ama unyenyekevu mbele za Mungu SHABAHA YA HII SIKU Kwet kama kanisa la kiinjili lakilutheri tumepewa mstari wakesho ambao ni Yoeli3:19a nakichwa ama wazo linasema KUTUBU NA KUREJEA KWA BWANA kwanza mkristo unatakiwa ujitathimini maisha yako je unaishi maisha yatoba ama unasubiri mpaka itokee kwenye kwaresma?? Kitu kingine mkristo anatakiwa ajifanyie hesabu ama tafakari fupi tokea kwarsma ya mwaka jana mapaka leo umesimama vizuri kwenye imani ambayo Yesu alituachia ama umekuwa mguu pande. KUTUBU NA KUREJEA KWA BWANA Ndugu zangu waamini …Bwana asifiwe tunapoanza majira haya ya toba siku 40 umejipangaje iliuwe kamili mbele za Mungu kumbuka yesu anatuambia “njoni kwangu nyinyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo ya dhambi nami nitawapumzisha” Mizigo mingapi inakulemea ndugu yangu kiasi kwamba hujapata mahali pakutua lakini yesu anatuambia utue kwake. Itaendelea kesho………@Evjohn